- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria Machi 15, 2023 imefanya ziara katika Manispaa ya Shinyanga, kwa kutembelea mradi wa ufunguzi wa barabara kilomita 2.5 ambao unatekelezwa na walengwa wa TASAF Mtaa wa Mwadui Kata ya Ngokolo wenye gharama ya TSh. milioni 25.6.
Kamati hiyo imeongozwa na Makamu Mwenyekiti, Florent Kyombo pia kuhudhuliwa na Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama, pamoja na Naibu Waziri Paulina Gikuli na Ridhiwani Kikwete.
Akizungumza kwenye ziara hiyo, Kyombo amesema amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo kutoka TASAF, unaoratibiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ambao fedha zimekuwa na mchango mkubwa kuchochea maendeleo, pamoja na kuzinyanyua Kaya Maskini kiuchumi.
"Miradi hii ya TASAF ambayo imekuwa ikiibuliwa na walengwa wa TASAF ikiwamo ya ufunguzi wa barabara napenda kutoa msisitizo kwa halmashauri, barabara hizi ziboreshwe na TARURA ili ziwe za kiwango kikubwa,. Naipongeza Manispaa ya Shinyanga kwa kuratibu vizuri mradi huu, ambao umekuwa chachu ya kuziinua kiuchumi kaya masikini" amesema Kyombo.
Kwa upande wake Waziri Mhagama amesema Serikali chini ya Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imekuwa ikitenga fedha nyingi kwa ajili ya walengwa wa TASAF na katika Bajeti ya iliyopita kimetengwa kiasi cha TSh. Bilioni 496 na kwa Mkoa wa Shinyanga zimepelekwa TSh. Bilioni 51.4
Amesema Ofisi yake itaendelea kusimamia fedha hizo za TASAF kwenye Program ya miradi ya jamii, ili maono ya Rais Samia yafikiwe na kuchochea maendeleo na kuziinua Kaya maskini kiuchumi na vilehilenakiipongeza Manispaanya Shinyanga, kwa kuutukia vizuri mradi wa ujenzi wa barabara ili kiuwasaidia walengwa wake.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo mkoani humo zikiwamo na fedha za walengwa wa TASAF Sh.bilioni 51.14 na miradi ya TASAF kwa mkoa mzima ipo 598, huku akiahidi kusimamia miradi hiyo na matumizi sahihi ya fedha.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga