- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
HERI YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inaungana na mataifa mengine ya Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 Juni 2025, ikiwa ni siku maalum ya kutafakari historia, kutathmini hali ya sasa, na kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha haki na ustawi wa watoto wetu zinalindwa na kuendelezwa.
Chimbuko la maadhimisho haya ni tukio la kihistoria la tarehe 16 Juni, 1976, lililotokea katika kitongoji cha Soweto, Afrika Kusini, ambapo watoto walijitokeza kupinga mfumo wa elimu wa kibaguzi, na kwa masikitiko makubwa, wengi wao waliuawa katika harakati hizo. Kupitia azimio la mwaka 1990, uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) uliitambua tarehe hiyo kama Siku ya Mtoto wa Afrika.
Katika kuenzi siku hii muhimu, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inawakumbusha wazazi, walezi, jamii nzima pamoja na wadau wa maendeleo kushiriki kikamilifu katika kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili, kuwapatia huduma bora za afya, elimu, malezi yenye maadili mema, na kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Taifa.
Katika Manispaa ya Shinyanga, tumeendelea kutekeleza mipango ya kimkakati ya kuimarisha ustawi wa mtoto kupitia utoaji wa huduma za afya na elimu, ulinzi wa mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, pamoja na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika malezi na maendeleo ya mtoto.
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2025 kitaifa yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Haki za Mtoto:Tulipotoka
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga