- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MRADI WA BOOST.
Na. Shinyanga Mc
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 1 Disemba, 2023 imepokea Cheti na Tuzo ya pongezi kwa utekelezaji mzuri wa Mradi wa BOOST katika hafla ya Tamasha la Bibititi Mohamed lililofanyika katika wilaya ya Rufiji, Mji mdogo wa Ikwiriri.
Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wananchi ikiongozwa na mgeni rasmi Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ambapo aliweza kutoa Tuzo na cheti cha pongeza kwa Halmashauri sita (6) zilizofanya vizuri katika utekelezaji mzuri wa Mradi wa Boost na Mradi wa sequip ambapo Kwa Manispaa ya Shinyanga imepokea Tuzo na Cheti cha pongezi kwa utekelezaji mzuri wa Mradi BOOST
Aidha, Manispaa ya Shinyanga iliweza kupokea Mradi wa BOOST katika shule mbalimbali za msingi ikiwemo shule mpya ya Msingi Ibadakuli B iliyojengwa kupitia Mradi wa BOOST kwa kujenga Madarasa ya Awali vyumba 2, Madarasa ya Msingi vyumba 14, Matundu ya vyoo 22, Jengo la Utawala pamoja na kichomea taka kwa gharama ya Shilingi Milioni 561,100,000/= iliyopelekea Manispaa ya Shinyanga kupata Tuzo na cheti cha pongezi.
Pamoja na mambo mengine kwa upande wa Manispaa ya Shinyanga Tuzo na cheti iliweza kupokelewa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa Mwl. Alexius Kagunze ambapo cheti kimoja ni pongezi kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ibadakuli kwa usimamizi mzuri wa Mradi wa BOOST.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga