- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, SHY MC
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Januari 18, 2023 ameweka Jiwe la Msingi katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga ambayo tayari imeshaanza kutoa huduma za Afya tangu Novemba 14, 2022.
Akifanya uzinduzi wa Hospitali hiyo iliyojengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu, Dkt. Mpango amesema ujenzi huo umefanyika ili kuhakikisha huduma za afya zinakuwa karibu na waanchi wa Shinyanga ili kurahisisha huduma badala ya kwenda mbali.
“Rais Samia amesikia kilio cha muda mrefu kwa watu wa Shinyanga, leo ameamua kutujengea Hospitali kubwa itakayowasaidia wananchi kutoenda sehemu zingine zaidi ya hapa kupata huduma, ni hatua kubwa ya maendeleo katika afya." amesema Dkt. Mpango.
Katika hatua nyingine Dkt. Mpango amewataka baadhi ya watumishi katika sekta ya afya kuacha kutumia lugha mbaya wanapotoa huduma kwa wagonjwa, akieleza ni kinyume na maadili ya kiapo cha kazi huku akitoa maagizo kwa wale watakaobanika kufanya hivyo wachukuliwe hatua za kisheria.
“Inasikitisha baadhi ya wauguzi wamekuwa wakitumia lugha mbaya kwa wagonjwa, kitu ambacho ni kinyuma na kiapo chao. Hatua zichukuliwe haraka kwa baadhi yao wanaofanya hivyo kwani inaondoa taswira chanya katika uwajibikaji wao”, amesema.
Aidha, kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga na Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Paschal Katambi, ametoa pongezi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mh. Jasinta Mboneko pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Jomaary Satura kwa Utendaji na Usimamiaji wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Idara ya Elimu, Afya, Miundominu na mingine katika Manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga