- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DKT. MAGEMBE ATEMBELEA NA KUKAGUA UTOAJI HUDUMA HOSPITALI YA MANISPAA NA KITUO CHA AFYA KAMBARAGE MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Naibu katibu Mkuu wa Afya Dkt. Grace Magembe leo tarehe 23 Februari, 2024 amefanya ziara Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kukagua miundombinu mbalimbali pamoja na kukagua namna huduma za afya zinavyotolewa katika hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na kituo cha afya kambarage.
Dkt. Magembe amepata wasaa wakukagua huduma zote zinazotolewa katika hospital ya Manispaa na kituo cha afya kambarage huku akiwapongeza wataalam kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi
“ Nipo katika ziara yenye lengo la kukagua miundombinu katika hospitali, vituo vya afya pamoja na namna huduma za afya zinavyotolewa kwa wananchi niwapongeze kwa kuendelea kutoa huduma nzuri hivyo, niwaombe muendelee kutoa huduma bora kwani Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwisha weka mazingira mazuri katika sekta ya afya na sekta zote kwa ujumla “ amesema Dkt. Magembe
Pamoja na mambo mengine Dkt. Magembe alipata wasaa wa kuongea na wataalam sekta ya afya na
Kuwasihi kuendelea kutoa huduma kwa kuzingia maadili, miongozo, taratibu na kanuni za utoaji wa huduma za afya huku akiwataka Mganga Mkuu wa Mkoa na Mganga Mkuu wa Manispaa kutoa motisha kwa wataalam wa afya wanaotoa huduma bora kwa wagonjwa ili kuendelea kuwapo moyo wa kuzidi kuhudumia wananchi vizuri.
Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa kwa niaba ya Mstahiki Meya Mhe. Zamda Mwebea amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Manispaa ya Shinyanga katika sekta zote hususani sekta ya afya kwani Shinyanga ya zamani na ya sasa katika sekta ya afya imezidi kuboreshwa zaidi.
Ziara hii ya Dkt. Magembe ni muendelezo wa ziara zake kwa lengo la kukagua miundombinu mbalimbali katika hospitali, zahanati na vituo vya afya pamoja na kukagua huduma za afya zinavyotolewa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga