- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC SAMIZI AWATAMBELEA WAHAWANGA WALIOBOMOLEWA NYUMBA KUFUATIA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo tarehe 2 Februari,2024 amewatembelea wahanga waliobomolewa nyumba kwa mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia tarehe 1 Februari , 2024 katika kata ya ndala, Mtaa wa ndala akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya pamoja na kamati ya maafa ya Manispaa ya shinyanga ambapo nyumba 33 zimebomolewa.
Akitoa pole kwa wananchi wa Ndala Mhe. Samizi amewataka wakazi wa ndala kuendelea kuchukua taadhari ya kutoka sehemu za mambondeni na kuondoka katika nyumba ambazo tayari zinahatarisha maisha kwa binadamu kwa kuwa tayari zimeshajenga nyufu na zengine kuloana kwa kiwango kikubwa.
“ Poleni sana ndugu kwa kupoteza nyumba na baadhi ya mifugo jukumu la serikali ni kulinda watu na mali zao hivyo niwaombe kwa nyumba ambazo tayari zinaviashiria vya kudondoka niwaombe muaze kutoka kwani serikali haipo tayari kupoteza watu kwa uzembe, hivyo niwaombe mtoke katika makazi hayo.”amesema Mhe Samizi
Pamoja na mambo mengine Mhandisi wa Manispaa Ndg. Kassimu Thadeo amewaeleza wananchi wa ndala kuwa nyumba za udogo wanazoishi tayari zimeshaloa na mvua , hivyo matofali yanakuwa yametanuka kwa kuloa , hivyo jua linapotoka sio kwamba itasaidia kukausha matofali hayo bali tofali husinyaa na kushindwa kuimiri uzito wa nyumba na kupelekea kubomoko hivyo ni vyema kuchukua tahadhari ya kutoka katika nyumba za namna hiyo ili kuepuka majanga makubwa zaidi.
Aidha , kamati za maafa kwa kila kata zinaendelea kutoa elimu na tahadhari juu ya mvua hizi zinazoendelea kunyesha, pia tayari wote walioathirika wameshapata hifadhi kwa majirani na ndugu wa familia.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga