- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC SAMIZI AFANYA KIKAO NA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA MITUMBA NGOKOLO MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo tarehe 5 Februari, 2024 amekutana na wafanyabiashara wa soko kuu la mitumba Ngokolo liliopo katika kata ya Ngokolo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mhe. Samizi amekutana na wafanyabiashara hawa kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali pamoja na kuwakumbusha sheria,na kanuni mbalimbali katika kuendesha biashara ya mitumba.
“ tumeitana hapa kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua kero mbalimbali pamoja na kukumbushana sheria, kanunia na taratibu katika uendeshaji wa biashara za mitumba.” amesema Mhe. Samizi
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Samizi aliwakaribisha wafanyabiashara waweze kutoa changamoto zao, ambapo waliwasilisha changamoto zikiwemo, kuomba uongozi wa Manispaa kupunguza ushuru wa meza na kuomba Manispaa kuendelea kuwatoa wafanyabiashara ambao hawapo sehemu rasmi za biashara ya mitumba na kurudishwa sehemu rasmi ambayo ni soko la ngokolo mitumbani.
Akijibu changamoto hizi Bi. Naely Somi Kaimu Mkuu Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ameeleza kwamba kupunguza ushuru wa meza na kuwa kiasi cha Tsh 20000 kwa mwaka ni jambo ambalo haliwezekani kutoka na sheria na taribu ambazo zimeshapangwa na badala yake ni kuendelea kulipa kiasi cha shilingi 10000/= kwa kila meza kwa mwezi mpaka pale utaribu mwengine utakapo wekwa huku akiwaomba wafanyabiashara kuwa wavumilivu kwani bado wanaendelea kutoa matangazo ya kuwatoa wafanyabiashara wote wa mitumba ambao hawapo sehemu rasmi na warudi katika soko kuu la mitumba ngokolo.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Samizi ameitaka ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya shinyanga kwenda kushughulikia changamoto zote walizowasilisha na wafanyabiashara hawa ili kuendelea kuleta maendeleo katika Manispaa na wananchi kwa ujumla.
Ziara hii ya Mhe. Samizi ni mwendelezo wa ziara zake kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali kwa wananchi.

Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga