- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC MTATIRO ASIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WAKAZI WA OLDSHINYANGA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. SHINYANGA Mc
MKUU wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro amesikiliza kero za wananchi wa Kata ya Oldshinyanga na kuzitatua,huku akiwataka watendaji wa Serikali wawe wanatatua kero za wananchi kwa wakati.
Mhe. Mtatiro amebainisha hayo leo Aprili 2, 2024 Kwenye Mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za Wananchi wa Kata hiyo, uliofanyika Viwanja vya Zahanati ya Oldshinyanga na kusema yupo Shinyanga kwa ajili ya kufanya kazi ya kumsaidia Rais Samia, katika kuwahudumia Wananchi na kutatua kero zao ambazo zinawakabili, na kuwataka Watendaji wa Serikali kwamba wakiletewa kero yoyote waitatue kwa wakati.
“Kazi yetu sisi ni kuhudumia Wananchi kumsaidia Rais Samia, na mimi sitakuwa Mkuu wa wilaya wa kukaa Ofisini,bali ni kiongozi wa Field na kuwafuata wananchi hukohuko kwenye maeneo yao na kuwapatia huduma,” amesema Mhe. Mtatiro.
“Kwenye eneo langu mimi la kazi nataka kila Jambo liwe limenyooka, ndiyo maana nafanya Mikutano ya hadhara ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, na kama Mwananchi unashida usisubili Mikutano tumieni namba yangu kunipigia 0739-420421 nipeni kero zenu nitazishughulikia,”ameongeza Mhe Mtatiro
Aidha amesisitiza kwa Watendaji wa Serikali ambao wanafanya kazi chini yake wajipange kisawasawa kufanya kazi kuwahudumia Wananchi, na kwamba wakizembea Matatizo yao atayapata kupitia namba yake ya Simu na atafika eneo husika kuitatua.
Nao baadhi ya Wananchi wa Oldshinyanga wametoa kero zao kwa Mkuu wa Wilaya,zikiwamo za Migogoro ya Mipaka, Urasimishaji maeneo,ukosefu Mashamba ya Kilimo,ulipwaji Fidia Mradi SGR, kuchelewa ulipwaji fidia kupisha ujenzi wa Barabara Kiwango cha Lami kutoka Oldshinyanga hadi Solwa, na hivyo kushindwa kufanya Shughuli zingine ikiwamo ujenzi wa nyumba, sababu tathimini imeshafanyika zaidi ya miaka miwili sasa.
Kero zote ambazo zimewasilishwa na wananchi zimepatiwa majibu na Wakuu wa Idara husika pamoja na Mkuu wa wilaya na kutatuliwa,pamoja na zingine kuahidiwa kufuatiliwa.
Ziara hii ya Mkuu wa Wilaya ni muendelezo wa ziara zake za kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga