• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Fedha
      • Ujenzi
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Hearth
      • Usafi na Mazingira
      • Land and Natural Resources
    • Vitengo
      • Tecknolojia, Habari, Mawasiliano na Uhusiano
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Nyuki na Maliasili
  • Fursa za Uwekezaji
    • Uwekezaji wa Viwanda
    • Fursa za kilimo
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Fursa za elimu
    • Fursa za Afya
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma za Ufugaji
    • Ufugaji wa Samaki
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma ya utoaji wa Mikopo
    • Kukondisha Vyumba vya Biashara
    • Unyonyaji wa Maji Taka
    • Huduma za Biashara
      • Leseni za Biashara
      • Elimu ya kibiashara
      • Ukaguzi wa Viwanda
      • Usimamizi wa Masoko
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Miundombinu
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya kamati za Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iIliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo za Halmashauri
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Mafunzo

DC MTATIRO ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI MWAMALILI MANISPAA YA SHINYANGA.

Posted on: July 8th, 2024

DC MTATIRO ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI MWAMALILI MANISPAA YA SHINYANGA.


Na. Shinyanga Mc


MKUU wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro,amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi Wamalili Manispaa ya Shinyanga na kuzitafutia ufumbuzi.


Mkutano huo umefanyika leo Julai 8,2024 kijijini humo na kuhudhuriwa na Watalaamu mbalimbali wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Taasisi za Serikali, ili kutoa majibu ya kero ambazo zitawasilishwa na wananchi kwenye mkutano huo.



Wakili Mtatiro akizungumza na wananchi hao,amesema ameletwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ili kumsaidia kazi ya kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na kutatua kero za wananchi.


“Nimeletwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hapa Shinyanga, kuja kurekebisha mambo sehemu ambazo zimepinda pinda na kulegea legea ili kupanyoosha, sasa hapa Mwamalili kuna baadhi ya Sekta mambo hayaende vizuri ndiyo maana nimekuja kusikiliza kero zenu ili nizitatue,”amesema Wakili Mtatiro.


Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Ndg. Said Kitinga akizungumza na wananchi kwenye Mkutano huo wakati akimkaribisha Mkuu wa wilaya kuzungumza na wananchi, ametoa wito kwa wananchi kwamba wajitume kufanya kazi ili wapate maendeleo kama alivyoelekeza Rais Samia, pamoja na kusomamesha watoto.


Kwa upande wake Diwani wa Mwamalili Mhe. James Matinde,amesema kwenye Kata hiyo Rais Samia ametoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na changamoto zilizopo zipo kwenye mchakato wa kutatuliwa likiwamo suala la ukosefu wa maji hasa katika kijiji cha Bushora.


Nao wananchi wakiwasilisha kero kwa Mkuu wa wilaya, wametaja baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili ikiwamo ya ukosefu wa huduma ya umeme,maji,upungufu wa Walimu, Wahudumu wa afya, kutolipwa fidia kwenye mradi wa SGR, ukosefu wa Josho la kuogeshea mifugo, na ubovu wa miundombinu ya barabara.

@ortamisemi

Tangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • Tazama

Habari Mpya

  • ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    May 08, 2025
  • MHE.MASUMBUKO AWATAKA MADIWANI KUSHIRIKIANA KIKAMILIFU KUKABILIANA NA WIZI WA VIFAA VYA MIRADI YA MAENDELEO.

    May 07, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MAAGIZO

    May 06, 2025
  • SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA SHULE YA WASICHANA SHINYANGA ILI KUIFANYA KUWA MIONGONI MWA SHULE BORA NCHINI “. NDG. MSIGWA.

    May 03, 2025
  • Tazama

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
Video Zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Ripoti mbalimbali
  • Sheria Ndogondogo za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Tovuti Nyingine tunazohusiana

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa(TAMISEM)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknologia
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Mkoa wa Shinyanga
  • Sekretarieti ya Ajira

wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Tanesco S, Mwanza Road

    Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga

    Simu: +255-28-2763213

    Simu ya Mkononi: 0759 023 788

    Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Ramani ya Tovuti
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga