- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Ndg. Said Kitinga Leo tarehe 31, Januari 2025 ameongoza mazoezi ya viungo vya mwili kwa watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni utekelezaji wa agizo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza kwenye mazoezi haya Ndg. Kitinga ameupongeza uongozi wa Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa na mwendelezo wa mazoezi Katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa, huku akitumia fursa hiyo kuwaasa wakazi wote wa Manispaa ya Shinyanga kuendelea kujitokeza Katika mazoezi haya ya kila mwisho wa mwezi ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Kwa upande wa wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambae pia ni Mkuu wa kitengo cha Utamaduni, sana na Michezo Ndg. Charles Luchagula amesema mazoezi haya ni endelevu kwa kila Mwezi.
“Tarehe 28 Mwezi wa pili tutafanya mazoezi kama haya, lakini mwisho wa mwezi wa tatu tutaandaa bonanza kubwa la michezo ambalo litashirikisha Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga lengo likiwa ni kutekeleza maagizo ya serikali Katika kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza”. Amesema Ndg. Luchagula.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga