- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Madiwani wake, imepitisha mapendekezo ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha (2023/2024) kiasi cha fedha Tsh. 36,848,918.000.00
Mapendekezo ya Bajeti hiyo yamepitishwa Januari 24, 2023 kwenye Mkutano Maalumu cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa (Lewis Kalinjuna), huku wakisisitiza kasi ya ukusanyaji mapato iendelee pamoja na kubuni vyanzo vipya ikiwamo ukusanyaji wa ushuru katika madini ya ujenzi.
Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ndg. Mensaria Humphray Mrema awali akisoma taarifa ya mapendekezo ya Mpango huo wa Bajeti wa mwaka wa fedha (2023/2024) amesema Manispaa inatarajia kukusanya kiasi cha fedha Tsh. Bilioni 36,848,918.000.00
“Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika mapendekezo ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha (2023/2024) tunarajia kukusanya na kutumia Tzs. 36,848,918.000.00 kwa mchanganuo ufuatao, vyanzo ya mapato ya ndani Tsh. Bilioni 6, ruzuku ya matumizi mengineyo Tsh. Milioni 738.6, ruzuku ya mishahara Tsh. Bilioni 21, Ruzuku ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali kuu Tsh. Bilioni 4.1 na Ruzuku ya miradi ya maendeleo wahisani Tsh. Bilioni 4.9.” alisema Mrema.
Kwa upande wao Waheshimiwa Madiwani kwa kauli moja walipongeza sana Menejimenti ya Manispaa inayoongozwa na Dkt. Jomaary Mrisho Satura ambaye ndiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kwa juhudi walizozionesha kwa kufanya kazi kwa weledi, maarifa, juhudi na uzalendo hata wakaweza kufanikiwa kuvuka lengo kwa mwaka wa fedha uliopita.
Lakini wakaonya kutojisahau na kubweteka kwa mafanikio hayo , badala yake waongeze juhudi zaidi ili lengo hili lililopishwa likayimie ikiwezekana na kuzidi kabisa na kuongeza umakini zaidi ikiwamo eneo la mapato ya madini ya ujenzi..
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias amewasihi watumishi ambao wanakusanya mapato waendelee kuwa na nidhamu ya fedha, pamoja na kutumia lugha nzuri wakati wa ukusanyaji mapato na kuhifadhi kanzi data, ili kubaini wafanyabiashara ambao wameshalipa mapato na kuondoa kero ya kuwafungia vibanda vyao na wakati walishalipa mapato.
“Bajeti ya mwaka wa fedha (2023/2024) tunakwenda kufanya vizuri zaidi, ila wale ambao mnahusika kwenye ukusanyaji wa mapato, tumieni lugha za weledi sababu watu hawa tunawahitaji ili walipe mapato, na fedha hizo ziendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi ikumbukwe kuwa sisi Manispaa na walipa mapato wetu tunao uhusiano mzuru sana tuendelee hivi hivi,” amesema Mhe. Masumbuko.
Na kwa upande wake muwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. John Tesha, amesema wataendelea kusimamia nidhamu kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani, pamoja na kufuatilia vyanzo vipya ikiwamo madini hayo ujenzi huku akimshukuru sana Rais wa Jamhurinya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha nyingi Manispaa ya Shinyanga.
Aidha, Resha alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Wilaya, Kamati ya Usalama, Mstahiki Meya, Madiwani, Menejimenti, watumishi na wadau wote kwa ushirikiano wao mkubwa na wenye tija na hata kuweza kufanikisha yote hayo.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga