- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MAAGIZO.
Na: Shinyanga MC
Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga limetoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya shinyanga, Mwl. Alexius Kagunze kwa utekelezaji wa maagizo waliotoa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili (Oktoba – Desemba 2024/25), hususani katika kushughulikia changamoto na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Pongezi hizi zimetolewa leo Mei 6, 2025, wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu kiichoketi kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ya kata zilizopo ndani ya Manispaa ya Shinyanga ambapo madiwani wameeleza kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Mkurugenzi katika kushughulikia changamoto zilizojitokeza kwenye kata zao, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya elimu, kutenga maeneo kwa ajili ya miradi ya huduma za kijamii, na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
“Mambo mengi yaliyokuwa changamoto kwenye kata zetu kwa kweli yametatuliwa. Wananchi wetu wanafurahia kazi nzuri inayofanywa na Halmashauri chini ya uongozi wa Mkurugenzi,” amesema Mhe. Dotto.
Miongoni mwa mafanikio yaliyobainishwa ni pamoja na utatuzi wa changamoto katika huduma za jamii na upangaji bora wa matumizi ya ardhi, ambapo Halmashauri imetenga maeneo maalum ili wananchi waweze kupisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa manufaa ya jamii.
Kwa upande wake, Msitahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Elias Masumbuko, amewahimiza madiwani kuendelea kusimamia suala la elimu, hasa katika kupambana na utoro mashuleni.
Akizungumza katika kikao hiki, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Alexius Kagunze amezipokea pongezi alizopewa na Madiwani na kuhaidi kuendelea kutatua changamoto pale zinapojitokeza huku akisema katika kipindi cha robo ya tatu, Serikali imefanikiwa kuajiri watendaji wa mitaa na vijiji vyote vilivyopo ndani ya Manispaa hii , jambo lililosaidia kutatua changamoto ya upungufu wa rasilimali watu na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga