- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
ALAT YAIPONGEZA MANISPAA YA SHINYANGA KWA UTEKELEZAJI MZURI UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.
Na. Shinyanga MC
Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Shinyanga wametembelea na kujionea utekelezaji wa mradi wa ujenzi jengo la utawala manispaa ya shinyanga linalojengwa katika kata ya Chamaguha, jengo linalogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 4 fedha kutoka serikali kuu.
Ziara hii ya ukaguzi imefanyika leo Mei 08, 2025 ikiongozwa na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Shinyanga Mhe. Mibako Mabubu ameupongeza uongozi wa manispaa ya shinyanga baraza la Madiwani pamoja na menejimenti kwa utekelezaji mzuri wa ujenzi uwo wenye kuzingatia thamani ya fedha iliyotolewa na serikali, huku akimshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutoa fedha katika kuboresha sekta mbalimbali pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa watumishi.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Kaimu mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu manispaa ya Shinyanga Ndg. Paschal Hyera amesema mradi huo unatarajia kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 4 ikihusisha ujenzi wa ofisi 41, kumbi mbili za mikutano, matundu 14 ya vyoo na vyumba 5 vya mifumo ya TEHAMA na kubainisha lengo la ujenzi wa jengo hilo.
“Lengo la mradi huu ni kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa kuondoa changamoto upungufu na uchakavu wa ofisi uliopo, jengo hili hadi sasa limetumia gharama ya Shilingi Bilioni 3.1 ambapo mpaka sasa limefikia asilimia 89 na kutarajia kukamilika ifikapo Disemba 30, 2025”, amesema Ndg. Hyera.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amesema kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo itapunguza adha ya watumishi kubanana ofisini kutokana na ufinyu wa majengo na kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga